Pages

Sunday, September 22, 2013

SIMBA SC ILIVYOKABWA KOO NA MBEYA CITY TAIFA LEO...DHAIRA HANA HAMU NA WALE WATOTO

Biashara gani hii; Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira akiwa amepiga magoti kipweke, baada ya Mbeya City kupata bao la kusawazisha na toa sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. 

Jonas Mkuse akigombea mpira wa juu na mchezaji wa Mbeya City

Winga wa Mbeya City, Deofratius Julius akiwatoka mabeki wa Simba SC

Amri Kiemba wakiwania mpira na Anthony Matogolo wa Mbeya City

Paul Nonga wa City akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Simba SC, Hassan Hatibu na Joseph Owino kulia

Betram Mombeki wa Simba kulia akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Mbeya City

Mombeki na mabeki wa Mbeya City

Mombeki na mabeki wa Mbeya City

Mombeki na mabeki wa Mbeya City

Mfungaji wa mabao mawili ya Simba SC leo, Amisi Tambwe akipambana na mabeki wa Mbeya City

Paul Nonga wa Mbeya City akimtoka Amri Kiemba wa Simba SC

Twaha Ibrahim wa Simba SC akimlamba chenga beki wa Mbeya City 

Paul Nonga wa Mbeya City akimtoka Amri Kiemba 

Hatari kwenye lango la Mbeya City

Wachezaji wa Mbeya City wakiomba dua kabla ya mechi

Twaha Ibrahim wa Simba akimpiga chenga beki wa Mbeya City

Haroun Chanongo wa Simba SC akifumua shuti mbele ya beki wa Mbeya City

Kikosi cha Mbeya City leo

Kikosi cha Simba SC leo

Benchi la Simba SC baada ya Mbeya City kusawazisha

Mashabiki wa Mbeya City waliosafiri kutoka Mbeya

Mashabiki wa Simba SC Taifa leo

Read more »

Saturday, September 21, 2013

Meneja wa wa klabu Liverpool Brendan Rodgers ameanza kuchonga kwa kutambia kuongoza EPL

Meneja wa wa klabu Liverpool Brendan Rodgers ameanza kuchonga kwa kutambia nafasi ya kwanza walioikalia katika msimamo wa ligi ya nchini Uingereza baada ya kufikisha point kumi.

Brendan Rodgers amesema ni mwanzo mzuri kwake pamoja na kikosi chake kwa ujumla na anafurahishwa na mwenendo walionao kwa sasa hivyo ana hakika mema na mazuri yanakuja zaidi.

Amesema wakati msimu huu ulipoanza kila mmoja alikua hana imani na kikosi chake kama kingeweza kufika katika nafasi waliopo sasa, lakini hana budi kuzungumza lolote la kutambia mazuri waliyoyafanya mpaka hii leo.

Brendan Rodgers ametambai nafasi ya kwanza waliokalia kwenye msimamo wa ligi, huku akiwa na mtihani mzito wa kuwakabili Southampton katika uwanja wa nyumbani wa Anfield hapo kesho.

Michezo mingine ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza itakayochezwa kesho itakua kati ya;


Carrow Road, Norwich
St James' Park, Newcastle


The Hawthorns, West Bromwich
Upton Park, London

Read more »

Bolt amesema huenda akashiriki michuano ya mbio za mita 200 pekee kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2014.



Mwanariadha anaetamba kwa wa mbio fupi duniani, Usain St Leo Bolt amesema huenda akashiriki michuano ya mbio za mita 200 pekee endapo ataamua kuwa miongoni mwa wanariadha watakaoelekea nchini Scotland kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2014.

Usain Bolt ambaye ni raia kutoka nchini Jamaica amesema maamuzi ya kushieriki michuano hiyo ambayo itafanyika kwenye jiji la Glasgow yatachangiwa na majadiliano aliyopanga kuyafanya na kocha wake Glen Mills kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Bolt mwenye umri wa miaka 27 amesema michuano hiyo ipo kwenye mipango yake na angependa kushiriki lakini hawezi lakini hawezi kufanya hivyo mpaka atakaposhauriana na kocha wake ambae anamuheshimu kwa kufuata anachomuelekeza.

Hata hivyo mwanariadha huyo amesema hata kama itatokea atakwenda kushiriki michuano ya Jumuia ya Madola bado angependa kushiriki katika mbio za mitya 200 kutokana na kuipenda mbio hizo zaidi.

Usain St Leo Bolt alifanikiwa kunyakuwa medali tatu za dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na mita 400 za kupokezana vijiti katika michuano ya olimpiki iliyofanyika mjini Beijing nchini China mwaka 2008 na kurudia tena katika michuano hiyo iliyofanyika jijini London nchini Uingereza mwaka 2012.

Read more »

TFF yajitetea kitendo cha Mchezaji wa Simba SC Khamis Tabwe kutopewa mpira baada ya kupachika mabao manne.


Shirikisho la soka nchini TFF limejitetea kufutia kitendo cha muamuzi alichezeshwa mchezo wa Simba na Mgambo Shooting Stars kushindwa kumzawadia mpira mshambuliaji Khamis Tabwe kama ishara ya kumbu kumbu baada ya kupachika mabao manne katika mchezo huo.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema muamuzi huyo hakufanya makosa kwa kushindwa kumzawadia mshambuliaji huyo kutoka nchini Burundi mpira, hivyo amewataka mashabiki kutambua hatua ya mchezaji kukabidhiwa mpira kama ishara ya heshima mara baada ya kufunga mabao matatu ama zaidi katika mchezo mmoja haipo kwenye kanuni na sheria za TFF ama FIFA.

Hata hivyo Boniface Wambura amesema bado TFF wanatambua umuhimu wa Khamis Tambwe kukabidhiwa mpira huo kaka ishara ya Fair Play na hivyo wanajipanga kufanya hivyo katika siku ambayo hakuitaja.

Hata hivyo kitendo cha Khamis Tambwe kunyimwa mpira mara baada ya mchezo dhidi ya Mgambo siku ya jumatano, kimewauma sana viongozi wa klabu ya Simba ambao walikuwepo kwenye uwanja wa taifa siku hiyo.

Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema kitendo hicho kimeufedhehesha mchezo wa soka la bongo hasa ikizingatiwa mchezaji alistahili kupewa heshima hiyo anatokea nje ya nchi.

Read more »

Saturday, September 14, 2013

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF, Leodegar Tenga ameishukuru Kamati ya ligi kwa usimamizi mzuri.


 Na Shaban Kondo Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF, Leodegar Tenga ameishukuru Kamati ya ligi kwa usimamizi mzuri tangu ilipokabidhi jukumu la kuisimamia ligi kuu katika mzunguko wa pili msimu uliopita.

Raisi Tenga amesema TFF iliamua kuanzisha Kamati hiyo kwa lengo la kutaka klabu zijisimamie zenyewe ili kuongeza ufanisi, jambo ambalo limeleta mabadiliko na kuondoka matatizo katika kuwalipa waamuzi na makamisha wanaosimamia michezo ya ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza.

Katika hatua nyingine rais Tenga amesema kamati hiyo pia imefanikiwa kutekeleza wajibu wa kudumisha utulivu na utawala bora na hivyo kusababisha kasi ya makampuni kutaka kuwekeza katika ligi kuu kuendelea kupewa nafasi kubwa.

Pia amesema kuanzia msimu ujao 2014/2015 klabu za Ligi Kuu hazitaruhusiwa kusajili wachezaji hadi zitakapowasilisha TFF ripoti zao za mapato na matumizi zilizokaguliwa (Audited accounts), hivyo klabu husika zijiandae kwa ripoti hizo za Januari hadi Desemba 2013.

Wakati huo huo, Rais Tenga amesema bado suala la tiketi za elektroniki linafanyiwa kazi na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo na liko katika hatua nzuri, kwani nia ya TFF na benki hiyo kuona kuwa linaanza haraka iwezekanavyo.

Read more »

Mbeya City kusuka au kunyoa dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Dar es salaam Young Africans.



Uongozi wa klabu Mbeya city umetangaza hali ya kikosi chao kuenedeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Dar es salaam Young Africans kama walivyofanya wakati wa mchezo wao wa pili dhidi ya maafande kutoka mkoani Pwani ruvu Shooting.



Mwenyekiti wa klabu hiyo inayocheza ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwake Mussa Mapunda amesema kikosi chao kipo tayari kupamabna na mabingwa hao kwa hali yoyote ile na kuhakikisha kimaliza dakika 90 kwa kuibuka na ushindi.



Nae kocha mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kesho ambao ana hakika utakua mgumu kutokana na uimara wa wapinzani wao.

Mchezo huo umepangwa kuchezeshwa na muamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani huku akitajwa kuwa ni James Mhagama kutoka mjini Songea mkoani Ruvuma.



Wakati Mbeya City wakiwakaribisha Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sokoine huko jijini Mbeya wekundu wa MSimbazi kesho watacheza kwa mara ya kwanz akatika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam baada ya kuanzia ugenini katika viwanja vya Ally Hassan mwinyi huko mkoani Tabora pamoja na kumbu kumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.



Simba watwakaribisha Mtibwa Sukari katika mchezo wa kesho huku wakiwa na kumbu kumbu ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata katiak mchezo uliopita dhidi ya JKT Oljoro huku wakata miwa kutoka Manungu Turiani mkoani Morogoro nao watakua wakichagizwa na ushidni kama huo walioupata mbele ya ndugu zao Kagera Sugar.



Afisa habari wa klabu ay Simba Ezekiel Kamwaga amesema maandalizi ya kikosi chao kuelekea katika mchezo wa kesho yamaeshakamilika hivyo amewataka mashabiki kujitokeza katika uwanja wa taifa kuishuhudia samba ikicheza kwa mara ya kwanza katika uwanja huo tangu msimu huu ulipoanza.



Viingilio katika mchezo huo utakaochezeshwa na muamuzi Dominic Nyamisana kutoka mkoani Dodoma vitakuwa sh. 5,000 viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.



Pia Azam TV itautumia mchezo huo kwa ajili ya mazoezi (broadcast training) kwa wafanyakazi wake. Hivyo mechi hiyo haitarekodiwa au kuoneshwa moja kwa moja.



Michezo mingine ya ligi kuu ya soka tanzani bara itakayochezwa kesho ni kati ya Coastal Union ambao wanarejea nyumbani katika uwanja wa Mkwakwani baada ya kuwalazimisha sare ya bao moja kwa moja Dar es salaam  Young Africans katika mchezo uliopita, kwa kucheza dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza kutoka jijini Mbeya Tanzania Prisons.



Kuelekea katika mchezo huo kocha mkuu wa Costal union Hemed Moroko amelitupia lawama shirikisho la soka nchini TFF kwa kushindwa kupanga mikakati mizuri ya kuziwezesha timu zinazoshiriki ligi kuu kuwa na mwenendo mzuri wa kuwatumia wachezaji wake ipasavyo.



Maafande wa Ruvu Shooting Ruvu Shooting kesho watakua katika uwanja wao wa Mabatini uliopo maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani wakiwakaribisha maafande wenzao kutoka wilaya ya handeni mkoani Tanga Mgambo Shooting.



Afisa habari wa Rucvu Shooting Masau Bwire amesema katika mchezo huo kikosi chao hakitokuwa tayari kurejea makosa ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City, hivyo kimefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuhakikisha kinapata point tatu muhimu.
 
Huko jijini Aerusha katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid wenyeji wa uwanja huo Oljoro JKT watacheza kwa mara nyingine nyumbani kwa kuwakabili Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora.



Katika uwanja wa Kaitba mkoani Kagera, waoka mikate jijini Dar es salaam Azam FC wataendelea kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi mbele ya wapinzani wao Kagera Sugar ambao bado hawajaionja tamu ya ushindi tangu msimu huu uliopoanza zaidi ya matokeo ya sare.



Nao Ashanti United watakua nyumbani jijini Dar es salaam wakicheza dhdii ya maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex.

Read more »

YANGA YAPEWA SIKU 14 KUWALIPA AKINA NSAJIGWA

 
 Mabingwa wa soka tanzani bara Dar es salaam Young Africans wamepewa siku 14 kuanzia hii leo kuhakikisha wanawalipa waliokuwa wachezaji wa klabu hiyo msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa pamoja na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka nchini TFF iliyokutana jana  ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.

Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba.

Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha wachezaji hao wawilia mbao walitemwa katika usajili wa msimu huu ambapo bado Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika anadai sh. milioni 6.5.

Wakati huo huo kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka nchini TFF imethibitisha usajili wa wachezaji 620 kati ya 624 wa timu za Ligi Daraja la Kwanza iliypangwa kuanza kuunguruma hapo kesho katika viwanja tofauti.

Wachezaji wanne ambao usajili wao umezuiwa mpaka watakapokamilisha taratibu ni Emmanuel Simwanza Namwando wa African Lyon, Godfrey Bonny Namumana (Lipuli FC), na Enyinna Darlington na Chika Keneth Chukwu wote wa Mwadui FC ya Shinyanga.

Darlington na Chukwu ambao wote ni Wanigeria wamezuiwa mpaka watakapowasilisha vibali vya kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji wakati Namumana aliyekuwa akicheza nchini Nepal bado hajapata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Nayo African Lyon imetakiwa kufikia muafaka na AYOSA Academy ambayo Namwando anatoka juu ya usajili kabla ya kuanza kumtumia mchezaji huyo.

Klabu ambazo zimemaliza nafasi zote 30 usajili katika FDL ni Friends Rangers FC ya Dar es Salaam, na Stand United FC ya Shinyanga wakati iliyosajili wachezaji wachache zaidi ni Burkina Faso FC. Klabu hiyo ya Morogoro imesajili wachezaji 19 tu.

Vilevile Kamati hiyo vilevile imethibitisha usajili wa wachezaji wanane wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) waliosajiliwa katika hatua ya pili ya usajili iliyoanza Agosti 14 hadi 30 mwaka huu.

Wachezaji hao ni Samir Ruhava na Amani Simba (Ashanti United), Robert Machucha na Said Ndutu (Yanga U20), Ayoub Masoud na Abdallah Selemani (Coastal Union U20), Ramadhan Kipalamoto (Simba U20) na Henry Joseph (Simba) ambaye tayari Hati yake Uhamisho wa Kimataifa (ITC) imeshawasili.

Read more »