Uongozi wa klabu Mbeya city umetangaza hali ya kikosi chao kuenedeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Dar es salaam Young Africans kama walivyofanya wakati wa mchezo wao wa pili dhidi ya maafande kutoka mkoani Pwani ruvu Shooting.
Mwenyekiti wa klabu hiyo inayocheza ligi kuu kwa mara ya kwanza
tangu kuundwa kwake Mussa Mapunda amesema kikosi chao kipo tayari kupamabna na
mabingwa hao kwa hali yoyote ile na kuhakikisha kimaliza dakika 90 kwa kuibuka
na ushindi.
Nae kocha mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi amesema kikosi chake
kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kesho ambao ana hakika utakua mgumu
kutokana na uimara wa wapinzani wao.
Mchezo huo umepangwa
kuchezeshwa na muamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani huku akitajwa kuwa ni James
Mhagama kutoka mjini Songea mkoani Ruvuma.
Wakati Mbeya City wakiwakaribisha Dar es salaam Young Africans
katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sokoine huko jijini Mbeya wekundu wa MSimbazi
kesho watacheza kwa mara ya kwanz akatika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
baada ya kuanzia ugenini katika viwanja vya Ally Hassan mwinyi huko mkoani
Tabora pamoja na kumbu kumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Simba watwakaribisha Mtibwa Sukari katika mchezo wa kesho huku
wakiwa na kumbu kumbu ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata
katiak mchezo uliopita dhidi ya JKT Oljoro huku wakata miwa kutoka Manungu
Turiani mkoani Morogoro nao watakua wakichagizwa na ushidni kama huo walioupata
mbele ya ndugu zao Kagera Sugar.
Afisa habari wa klabu ay Simba Ezekiel Kamwaga amesema maandalizi ya kikosi chao kuelekea katika
mchezo wa kesho yamaeshakamilika hivyo amewataka mashabiki kujitokeza katika
uwanja wa taifa kuishuhudia samba ikicheza kwa mara ya kwanza katika uwanja huo
tangu msimu huu ulipoanza.
Viingilio katika mchezo huo utakaochezeshwa na muamuzi Dominic
Nyamisana kutoka mkoani Dodoma vitakuwa sh. 5,000 viti vya bluu na kijani, sh.
8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh.
20,000.
Pia Azam TV itautumia mchezo huo kwa ajili ya mazoezi (broadcast
training) kwa wafanyakazi wake. Hivyo mechi hiyo haitarekodiwa au kuoneshwa
moja kwa moja.
Michezo mingine ya ligi kuu ya soka tanzani bara itakayochezwa
kesho ni kati ya Coastal Union ambao wanarejea nyumbani katika uwanja wa
Mkwakwani baada ya kuwalazimisha sare ya bao moja kwa moja Dar es salaam Young Africans katika mchezo uliopita, kwa
kucheza dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza kutoka jijini Mbeya Tanzania
Prisons.
Kuelekea katika mchezo huo kocha mkuu wa Costal union Hemed Moroko
amelitupia lawama shirikisho la soka nchini TFF kwa kushindwa kupanga mikakati
mizuri ya kuziwezesha timu zinazoshiriki ligi kuu kuwa na mwenendo mzuri wa
kuwatumia wachezaji wake ipasavyo.
Maafande wa Ruvu Shooting Ruvu Shooting kesho watakua katika
uwanja wao wa Mabatini uliopo maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani wakiwakaribisha
maafande wenzao kutoka wilaya ya handeni mkoani Tanga Mgambo Shooting.
Afisa habari wa Rucvu Shooting Masau Bwire amesema katika mchezo
huo kikosi chao hakitokuwa tayari kurejea makosa ya kupoteza mchezo uliopita
dhidi ya Mbeya City, hivyo kimefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya
kuhakikisha kinapata point tatu muhimu.
Huko jijini Aerusha katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sheikh Kaluta
Amri Abeid wenyeji wa uwanja huo Oljoro JKT watacheza kwa mara nyingine
nyumbani kwa kuwakabili Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora.
Katika uwanja wa Kaitba mkoani Kagera, waoka mikate jijini Dar es
salaam Azam FC wataendelea kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha wanaendeleza
wimbi la ushindi mbele ya wapinzani wao Kagera Sugar ambao bado hawajaionja
tamu ya ushindi tangu msimu huu uliopoanza zaidi ya matokeo ya sare.
Nao Ashanti United watakua nyumbani jijini Dar es salaam wakicheza
dhdii ya maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex.
0 comments:
Post a Comment