Mwanariadha anaetamba kwa wa mbio fupi duniani, Usain St Leo Bolt amesema huenda akashiriki michuano ya mbio za mita 200 pekee endapo ataamua kuwa miongoni mwa wanariadha watakaoelekea nchini Scotland kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2014.
Usain Bolt ambaye ni raia kutoka
nchini Jamaica amesema maamuzi ya kushieriki michuano hiyo ambayo itafanyika
kwenye jiji la Glasgow yatachangiwa na majadiliano aliyopanga kuyafanya na kocha
wake Glen Mills kabla ya kutoa
uamuzi wa mwisho.
Bolt mwenye umri wa
miaka 27 amesema michuano hiyo ipo kwenye mipango yake na angependa kushiriki
lakini hawezi lakini hawezi kufanya hivyo mpaka atakaposhauriana na kocha wake
ambae anamuheshimu kwa kufuata anachomuelekeza.
Hata hivyo mwanariadha huyo amesema
hata kama itatokea atakwenda kushiriki michuano ya Jumuia ya Madola bado
angependa kushiriki katika mbio za mitya 200 kutokana na kuipenda mbio hizo
zaidi.
Usain St Leo Bolt
alifanikiwa kunyakuwa medali tatu za dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na
mita 400 za kupokezana vijiti katika michuano ya olimpiki iliyofanyika mjini Beijing
nchini China mwaka 2008 na kurudia tena katika michuano hiyo iliyofanyika
jijini London nchini Uingereza mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment