Majina ya mameneja Roberto
Di Matteo , Tony Pulis , Gus Poyet , Alex McLeish pamoja na Steve
McClaren yamekua yakitajwa katika mchakato wa kumsaka mrithi
wa meneja kutoka nchini Italia Paolo Di Canio ambae amefungashiwa virago huko Stadium of Light
yalipo makao makuu ya klabu ya Sunderland.
Vyombo vya habari nchini
Uingereza tangu mapema hii leo vimekua vikiyataja majina ya mameneja hao ambao
wanaijua vyema ligi ya nchini humo kwa kusema huenda mmoja wao akapewa ajira na
uongozi wa klabu ya Sunderland.
Taarifa hizo zimedai kwamba
mameneja wote hao wamekua katika harakati za kutafuta kazi kwa muda wa miezi
kadhaa sasa na wapo tayari kuichukua nafasi ya Paolo Di Canio ambae ameionja shubiri ya kutimulia kazi baada ya
kushindwa kuanza vyema msimu wa ligi nchini Uingereza.
Hata hivyo katika mlolongo wa
mameneja hao Roberto
Di Matteo, ambae aliiwezesha klabu ya Chelsea kuandika historia ya kuwa
wafalme wa soka mwaka 2012 barani Ulaya, anaonekana kuwa chaguo la kwanza la
viongozi wa klabu ya Sunderland ambao bado wanaendelea kujadiliana namna ya
kuiziba nafasi ya meneja klabuni hapo.
Paolo
Di Canio ambae alipewa
ajira huko Stadium of Light mnamo March 31 mwaka huu alifanikiwa kuinusuru
klabu ya Sunderland kushuka daraja msimu uliopita baada ya kuikuta ikiwa katika
hali mbaya ambayo ilisababishwa na utendaji mbovu wa meneja aliemtangulia Steve Bruce.
Tangu
alipoingia klabuni Paolo
Di Canio mwenye umri wa miaka 45,
alifanikiwa kushinda michezo mitatu pekee kati ya michezo 13 ambayo
imeshuhudiwa ikichezwa akiwa kama mkuu wa benchi la ufundi.
Akizungumza mara baada ya mchezo
wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya West Bromwich Albion ambao ulikua
mchezo wa mwisho kwake kama meneja wa klabu ya Sunderland Paolo Di Canio alikiri kikosi chake bado kilikua na matatizo ya kuelewana
baina ya mchezaji na mchezaji hivyo ilikua ni vigumu kwake kuanza vyema msimu
huu huku wakiwa tayari wameshacheza michezo mitano.
Pia Paolo Di Canio akajitabiria mabaya wakati alipokua akizungumza na
vyombo vya habari kwa kusema yeye alistahili kuwajibishwa kwa kosa hilo.
Katika
mchezo huo kikosi cha Sunderland kilikubali kisago cha mabao matatu kwa sifuri,
na kabla ya hapo walikubali kufungwa na Arsenal mabao matatu kwa moja huku
Cryastal palace wakitanguli
0 comments:
Post a Comment