Shirikisho la soka nchini TFF limejitetea kufutia kitendo
cha muamuzi alichezeshwa mchezo wa Simba na Mgambo Shooting Stars kushindwa
kumzawadia mpira mshambuliaji Khamis Tabwe kama ishara ya kumbu kumbu baada ya
kupachika mabao manne katika mchezo huo.
Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema muamuzi huyo
hakufanya makosa kwa kushindwa kumzawadia mshambuliaji huyo kutoka nchini
Burundi mpira, hivyo amewataka mashabiki kutambua hatua ya mchezaji kukabidhiwa
mpira kama ishara ya heshima mara baada ya kufunga mabao matatu ama zaidi
katika mchezo mmoja haipo kwenye kanuni na sheria za TFF ama FIFA.
Hata hivyo Boniface
Wambura amesema bado TFF wanatambua umuhimu wa Khamis Tambwe kukabidhiwa mpira
huo kaka ishara ya Fair Play na hivyo wanajipanga kufanya hivyo katika siku
ambayo hakuitaja.
Hata hivyo kitendo cha
Khamis Tambwe kunyimwa mpira mara baada ya mchezo dhidi ya Mgambo siku ya
jumatano, kimewauma sana viongozi wa klabu ya Simba ambao walikuwepo kwenye
uwanja wa taifa siku hiyo.
Afisa habari wa klabu
ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema kitendo hicho kimeufedhehesha mchezo wa soka
la bongo hasa ikizingatiwa mchezaji alistahili kupewa heshima hiyo anatokea nje
ya nchi.
0 comments:
Post a Comment