Viboko wa ajabu
Katika Kijiji cha Makangaga, kilometa tisa kutoka kijijini hapo, kuna
Mto Nyange uliosheheni viboko wa ajabu ambao wana tabia ya ‘kucheka’ na
kutii amri zinazotolewa, hakika ukifika unajua wamefundishwa, ni fursa
nzuri ya utalii kama itatumiwa vyema.
Majira ya usiku viboko hao wanapenda kutembea kando ya maeneo yao kwa
ajili ya kujipatia vyakula na sehemu kubwa wanakula majani na pia wana
tabia za ziada.
Zaidi ya miaka 100 iliyopita mto huo uliotengeneza bwawa na haukuwa na
kiboko hata mmoja, wakazi wa maeneo hayo walitumia bwawa hilo kwa
shughuli za uvuvi na mahitaji ya maji kwa kazi za kawaida.
Mkazi wa eneo hilo Yahaya Selemani Engema anaeleza chanzo ni mkazi mmoja
aliyetajwa kwa jina la Kimombo ambaye alikuwa mvuvi hodari kwenye bwawa
hilo.
Lakini siku moja alipokwenda kuvua hakurejea na historia kuanzia hapo baada ya wananchi kuona kiboko mmoja kwenye bwawa hilo.
“Ndugu zake baada ya kusubiri kwa siku sita wakiamini atarejea, waliamua
kwenda bwawani hapo kwa nia ya kumtafuta, walimwita kwa kutumia lugha
ya kabila la Wamachinga, ajabu baada ya kutokea Kimombo kama
walivyotarajia alitokea kiboko ambaye alicheka kama ishara ya kuitika,
kutokana na hali hiyo ndugu wa familia ya mvuvi huyo waliamini ndugu yao
alizama kwenye bwawa hilo na kubadilika kuwa kiboko ambao wanatabia ya
kucheka,”anasema Omari Yanda mmoja wazee maarufu kijiini hapo.
Kila mwaka hivi sasa inakadiriwa kuwa wanafikia zaidi ya viboko 300, na kwamba wanatii amri ya ukoo wa Kimombo.
“Familia iliyoshikilia wanyama hao ni ya Kimombo wanarithishana kwa kuwa
kiboko wa kwanza alitoka katika familia hiyo, wageni wanaofika kuwaona
viboko hao huwaita viboko hao kwa kutumia jina la Kimombo ndipo viboko
hao hujitokeza wakicheka,” anasema Yanda.
Miongoni mwa maajabu ya viboko hao ni kuwa wana uwezo wa kujitokeza
pindi wanapohitajika kwa maana wakitakiwa wajitokeze wadogo wataibuka
wadogo na wakitakiwa wajitokeze wazee watajitokeza wazee wote waliomo
bwawani.
0 comments:
Post a Comment