****
Wakati kamati ya rufaa ya maadili ikitarajia kukutana leo
kwa ajili ya kusikiliza rufaa zilizowasilishwa mbele yake pamoja na kutoa
ufafanuzi wa maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya maadili majuma mawili
yaliyopita dhidi ya wadau wa soka waliotakiwa kuendelea na adhabu ya kuenguliwa
katika mchakato wa uchaguzi mara baada ya kusikilizwa kwa mashauri yao,
shirikisho la soka nchini TFF imeendelea kutoa ufafanuzi wa nini na nani yupo
katika familia ya soka.
Mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji Alex
Mgongolwa amesema tafsiri wa nini na nani yupo katika familia ya soka imekua
ikitolewa tafsiri tofauti ambapo hali hiyo inaleta mkanganyiko na kusababisha
baadhi ya wadau walioenguliwa katika mchakato wa uchaguzi kujiona hawana haki
ya kuwa katika familia hiyo.
Bofya hapa chini kumsikiliza:- MGONGOLWA
Hata hiyo kwa kuonyesha ni vipi suala hilo linavyowachanganya wadau wa soka nchini, bado raisi wa shirikisho la soka
nchini TFF Leodger Chilla Tenga alipokutana na waandishi wa habari siku mbili
zilizopita alizungumza kwa lengo la kufafanua nini chanzo cha kuundwa kwa
kamati za maadili kama ilivyoagizwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
Bofya hapa chini kumsikiliza:- RAIS WA TFF TENGA
0 comments:
Post a Comment