Pages

Tuesday, June 25, 2013

HAKIKA WATANZANIA WANA KIU KUBWA YA KUONA TABASAMU LAKO.



 Marehemu Amina Chifupa.
NAMKUMBUKA KWA TABASAMU LAKE,UCHESHI WAKE,SAUTI YAKE NZURI IKIPENYA KTK MASIKIO YA WASIKILIZAJI WAKE ALIPOKUWA PALE CLOUDS FM KAMA MTANGAZAJI,LAKI NI GHAFLA AKAWA MBUNGE NA MWANAHARAKATI MACHACHALI KILA MTU ALIMJUA KUTOKANA NA UAMUZI MGUMU ALIOCHUKUA WA KUTAKA  KUWATAJA WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

..MMH...!! BILA SHAKA UMESHAPATA PICHA NAMZUNGUMZIA NANI.. SI MWINGINE NI MAREHEMU AMINA CHIFUPA.

MAREHEMU AMINA ALIKUWA MWANAMKE NA MBUNGE WA KWANZA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU YA KUTAKA KUWATAJA WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA HAPA NYUMBANI TZ... WENGI TULISUBIRI KWA HAMU SIKU HIYO LAKINI KWA BAHATI MBAYA AKAFARIKI SIKU HIYO HIYO YA AHADI YAKE (26/06/2007) HATUA YA AMINA KUTAKA KUWATAJA WATU HAWA PENGINE INGESAIDIA KUPUNGUZA KAMA SIO KUMALIZA KABISA TATIZO LA UTUMIAJI WA DAWA HIZO HARAMU AMBAZO ZIMEATHIRI VIJANA WENGI.

 OKEY...NIMEBAKI NA SWALI JE NANI ANAYEWEZA KUPAZA SAUTI KUWATAJA ..!!??/MIMI NA WEWE TUNAWEZA KWA NJIA TOFAUTI,HUKU TUKIMKUMBUKA AMINA LEO /SAY NO TO DRUGS/

REST IN PEACE AMINA CHIFUPA

Read more »

Monday, June 24, 2013

::::: TUZO ZA SOKA ZILIZOTOLEWA NA SPUTANZA :::::;

AMRI KIEMBA
Chama cha wachezaji wa soka nchini SPUTANZA kwa udhamini wa Peps mwishoni mwa juma lililopita kilifanikisha azma ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji pamoja na makocha waliofanya vyema katika msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2012-13.

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, ilishuhudia wadau wachache wakijitokeza, hali ambayo imepokelewa tofauti na uongozi wa SPUTANZA kwa kukiri japo ni mwanzo wameona walifanya makosa katika utaratibu wa kuitangaza siku hiyo.

Katibu mkuu wa SPUTANZA Said George amesema watayafanyia kazi mapungufu hao kwa kiasi kikubwa ili hafla ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji na makocha watakaofanya vizuri msimu ujao iweze kufana.

Katika hafla hiyo inayojulikana kama SPUTANZA FOOTBALL AWARDS wachezaji watatu pamoja na kocha mmoja walizawadiwa baada ya kujizolea kura nyingi zilizopigwa na jopo la makocha.
Tujikumbushie namna ambavyo washindi walivyo tangazwa
1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu - Amri Kiemba (Simba)
Amewashinda
Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu (Yanga),
Kipre Tchetche (Azam),Paul Nonga (Jkt Oljoro)

2. Kocha Bora wa Mwaka - Mecky Maxime (Mtibwa Sugar)
Amewashinda
Boniface Mkwasa (Ruvu shooting),Abdallah Kibaden (Kagera Sugar) Jumanne Charles (Prisons)

3. Mchezaji Bora Chipukizi - Salum Abubakar "Sure Boy" (Azam)
Amewashinda
Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Issa Rashid (Mtibwa)
Shomari Kapombe (Simba) Twaha Shekue (Coastal Union)

4. Golikipa Bora - Hussein Sharif "Casilas" (Mtibwa Sugar)
Amewashinda
Juma Kaseja (Simba), Mwadin Ally (Azam).

Zawadi ya mchezaji bora wa msimu uliopita imekwenda kwa ya kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa Taifa Stars pamoja na klabu ya Simba Amri Kiemba.

Hata hivyo cha kushangaza tuzo ya mchezaji huyo ilipokelewa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ay Dar es salaam Young Africans Mohammed Binda ambae akatoa siri ya kumuwasilisha Amri kiemba.

Read more »

Sababu za Chadema kususia kuhudhuria kikao cha bunge June 24 2013

.
.
Kutokana na viongozi wakuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuzuiwa kuingia ndani ya bunge wakiwa wamevaa sare za chama, wabunge wa Chadema wamesusia kuhudhuria kikao cha kupitisha bajeti ya serikali 2013/14 jioni hii ya June 24 2013.
Huo uamuzi umetangazwa na mnadhimu mkuu wa kambi hiyo Tundu Lissu ambapo  amesema ni kinyume na kanuni ya bunge inayozungumzia mavazi rasmi ya wabunge wanaume.
Arusha mabomu june 18 2013
 
Namkariri Tundu Lissu akisema “Tumeona hatuwezi kushiriki katika shughuli ya bunge ya leo, tunakwenda kushiriki nini? kufanya uamuzi wa aina gani? wakati hatujashiriki kwenye mjadala kwenye mjadala kwa sababu ambazo tumezieleza, hatuwezi tukaingia bungeni kupiga kura kuamua kitu ambacho hatukukijadili, tumezuiwa kukijadili, tukio la bomu la Olasiti Arusha Mh Spika aliongoza ujumbe wa Wabunge karibu 30 kwenda kuwapa pole na kuangalia eneo la tukio, this time watu wameumizwa, watu wamekufa, bunge halijaahirisha shughuli halitoa mchango hata senti kumi na hakuna hata wazo la kwenda kuwaona walioumia na waliofiwa”
Kwenye sentensi nyingine, Tundu Lissu ameonyesha kushangazwa na bunge kuendelea na majadiliano ya uchumi wa Taifa 2012 na mpango wa maendelea ya Taifa 2013/2014 wakati kukiwa na tukio la mauaji lililotokea Arusha ambapo watu watatu walifariki dunia.
Hata hivyo wakati Chadema wakisusia kikao cha bunge, wabunge wengine walikua wanatarajia kuipitisha bajeti hiyo ya Serikali ya 2013/14 iliyotenga zaidi ya Trillioni 18.2 (kwa hisani ya Millardayo.com)

Read more »

Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba zinazoingizwa kwenye soko la hapa nchini.

Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba zinazoingizwa kwenye soko la hapa nchini.

Msemaji wa shirika la viwango TBS Bi. Rhoida Andusamile amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya agizo la sheria ya 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani zilizokwisha tumika.

 Lakini licha ya unafuu wa gharama za upatikanaji wa nguo za mitumba Nchini, Serikali kupitia TBS imepiga
marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo hizo ikiwemo soksi na nguo za kulalia zoezi linalohusisha Nchi nzima.

Mara nyingi nguo za ndani za mitumba zimekuwa zikitumiwa na jinsia zote mbili lakini wanawake ndiyo wameonekana kuwa wateja wakubwa wa nguo hizo wao walikuwa na maoni gani juu ya kupigwa marufuku uuzwaji wa ngao hizo?.

Kwa upande wao wauzaji wa nguo hizo walikuwa na maneno ya kuongea "Hii ni mara ya pili kwa
Shirika la viwango Tanzania - TBS kupiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba, lakini bado biashara hiyo imekuwa ikishamiri kwa kasi.

 #source-Star Tv#

Read more »

Thursday, June 20, 2013

Mabondia wa Tanzania wafungwa Mauritius

Mabondia waliohukumiwa.

Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.

 Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.

Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.

"Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema

Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.

Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.

Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

Read more »

BINGWA WA OLIMPIKI AKAMATWA UFARANSA KWA KOSA LA KUWAIBA WANAWE

Khalid ametuhumu serikali ya Norway kwa kuwaiba wanawe kutoka Morocco

Bingwa wa michezo ya olimpiki kutoka nchini Morocco, anayedai kuwa wanawe, waliibwa na mawakala wa Norway , amekamatwa nchini Ufaransa.

Khalid Skah, aliyeshinda mbio za mita 10,000, michezo ya Olimpik ya Barcelona 1992, alizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Orly mjini Paris, baada ya kusakwa na maafisa wa Norway kwa kosa la kuwaiba wanawe.

Kwa miaka mingi, amekuwa akilumbana na mkewe raia wa Norway mahakamani kuhusu nani anayepaswa kuwalea wanao.

Kesi hii imesababisha mzozo wa kidiplomasia baada ya Norway kukubali kuwa ilihusika na mpango wa kuwahamisha watoto hao kutoka Morocco.

Bwana Skah alithibitisha kukamatwa kwake kupitia mtandao wa kijamii.

Wakili wake wa Norway, Brynjar Meling, anasema kuwa bwana Skah ameomba atibiwe lakini yuko tayari kusafiri kwenda Norway kuweza kujieleza kwa maafisa wa nchi hiyo.

Bwana Skah, amekuwa akiwashtumu maafisa katika ubalozi wa Norway nchini Morocco, kwa 'kuwateka nyara' wanawe na kumsaidia mkewe Anne Cecilie Hopstock, kuwachukua kinyume na sheria.

Aidha Hopstock alikwenda Morocco na familia yake mwaka 2006, lakini akarejea mnamo mwaka 2007 baada ya uhusiano wake na mumewe Skah kuvunjika.

Watoto hao, Tarik na Selma, walisalia Morocco, lakini wakatoweka nyumbani kwao mwaka 2009 na mnamo mwaka 2010 walioenekana kwa mara nyingine katika televisheni ya Norway.

Vijana hao walisimulia walivyotoroka nyumbani kwao baada ya babao kuwa mkali kiasi cha kuwafungia ndani ya vyumba vyao.

Waliwasiliana na mama yao ambaye naye aliwasiliana na ubalozi wa Norway mjini Rabat kutaka usaidizi.

Maafisa katika ubalozi huo walifanya mipango ya kuwachukua watoto hao kutoka barabarani na kuwapa hifadhi katika makao ya ubalozi ambako walisalia hadi waliposafirishwa kwenda uhispania kwa ndege.

"Sisi wenyewe ndio tulitaka kutoroka," alisema Tarik.

Selma aliongeza kusema: "hatukuruhisiwa kuishi maisha ya kawaida wala hatukuruhusiwa kwenda shuleni."
Norway ilikubali kuwa mmoja wa maafisa wake aliwasaidia watoto wake akishirikiana na afisaa mmoja wa kikosi maalum aliyewasafirisha watoto hao kutoka Morocco.

Serikali ya Morocco imewatuhumu maafisa wa Norway kwa kukiuka mkataba wa Vienna kuhusu maswala ya kidiplmoasia na kutaka washtakiwe.

Bwana Skah na Bi Hopstock wote wameruhusiwa kuwalea wanao kila mmoja nchini Kwake ingawa sasa wanasemekana kuwa watu wazima wanaoweza kufanyia maamuzi.

 #Source BBC

Read more »

Viboko wa ajabu wasiojulikana kwa watalii

 




Wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 1525 wanaotokana na makabila ya Wamwera, Wangindo, Wamakonde, na Wamachinga ambao wanalitumia eneo hilo kama kivutio cha utalii ambalo linachangia pato la wakazi wa eneo hilo mpaka taifa kutokana na watalii wa ndani na nje.
Viboko wa ajabu
Katika Kijiji cha Makangaga, kilometa tisa kutoka kijijini hapo, kuna Mto Nyange uliosheheni viboko wa ajabu ambao wana tabia ya ‘kucheka’ na kutii amri zinazotolewa, hakika ukifika unajua wamefundishwa, ni fursa nzuri ya utalii kama itatumiwa vyema.
Majira ya usiku viboko hao wanapenda kutembea kando ya maeneo yao kwa ajili ya kujipatia vyakula na sehemu kubwa wanakula majani na pia wana tabia za ziada.
Zaidi ya miaka 100 iliyopita mto huo uliotengeneza bwawa na haukuwa na kiboko hata mmoja, wakazi wa maeneo hayo walitumia bwawa hilo kwa shughuli za uvuvi na mahitaji ya maji kwa kazi za kawaida.
Mkazi wa eneo hilo Yahaya Selemani Engema anaeleza chanzo ni mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Kimombo ambaye alikuwa mvuvi hodari kwenye bwawa hilo.
Lakini siku moja alipokwenda kuvua hakurejea na historia kuanzia hapo baada ya wananchi kuona kiboko mmoja kwenye bwawa hilo.
“Ndugu zake baada ya kusubiri kwa siku sita wakiamini atarejea, waliamua kwenda bwawani hapo kwa nia ya kumtafuta, walimwita kwa kutumia lugha ya kabila la Wamachinga, ajabu baada ya kutokea Kimombo kama walivyotarajia alitokea kiboko ambaye alicheka kama ishara ya kuitika, kutokana na hali hiyo ndugu wa familia ya mvuvi huyo waliamini ndugu yao alizama kwenye bwawa hilo na kubadilika kuwa kiboko ambao wanatabia ya kucheka,”anasema Omari Yanda mmoja wazee maarufu kijiini hapo.
Kila mwaka hivi sasa inakadiriwa kuwa wanafikia zaidi ya viboko 300, na kwamba wanatii amri ya ukoo wa Kimombo.
“Familia iliyoshikilia wanyama hao ni ya Kimombo wanarithishana kwa kuwa kiboko wa kwanza alitoka katika familia hiyo, wageni wanaofika kuwaona viboko hao huwaita viboko hao kwa kutumia jina la Kimombo ndipo viboko hao hujitokeza wakicheka,” anasema Yanda.
Miongoni mwa maajabu ya viboko hao ni kuwa wana uwezo wa kujitokeza pindi wanapohitajika kwa maana wakitakiwa wajitokeze wadogo wataibuka wadogo na wakitakiwa wajitokeze wazee watajitokeza wazee wote waliomo bwawani.

Read more »

Tuesday, June 18, 2013

Nukuu 5 za Serikali kuhusu zawadi kwa atakayefanikisha Mtuhumiwa bomu la Arusha kukamatwa na mengine.

.
.
Zifuatazo ni nukuu za maneno yaliyotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, sera, uratibu na bunge William Lukuvi kuhusu hilo bomu ambalo lililipuliwa kwenye mkutano cha Chadema Arusha.

“Mtu asiejulikana alirusha kitu katika kundi la watu kilichosababisha mlipuko mkubwa, mkutano huu ulikua na ulinzi wa jeshi la Polisi wakiwa na magari mawili… askari walisimama upande wa Kaskazini ya uwanja ambapo mrushaji alikua mashariki na alirusha bomu kuelekea Magharibi”

“Jaribio la Askari Polisi kutaka kumfata alierusha lilizuiwa na makundi ya Wananchi ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na kuwazomea na hivyo Polisi kulazimika kuanza kujiokoa badala ya kumsaka Muhalifu”

“Mlipuko huo ulisababisha watu wawili kufariki dunia ambao ni Judith William (48) na mtoto Ramadhan Juma (15) na watu 70 wamejeruhiwa miongoni mwao watatu wamejeruhiwa vibaya na wawili hali zao ni mbaya”

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mlipuko huo ulikuwa ni wa bomu la kurusha kwa mkono ambapo pia aina ya urushaji wa bomu hilo haitofautiani na mbinu iliyotumika kwenye shambulio jingine la bomu lililotokea kwenye kanisa la Olasiti Arusha”

“Kutokana na mfululizo wa matukio haya mageni, Serikali imeamua kutenga shilingi milioni 100 kama zawadi kwa mtu yeyote atakaeshirikiana na kutoa taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa muhalifu wa  matukio ya aina hii na mtandao wake mzima”

Read more »

NMB wametisha!! wamezindua kitu kinaitwa Chap chap akaunti kwa ajili ya Watanzania wasio na akaunti

..
Mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma

Benki ya NMB inaendelea kumiliki headlines kwa kubuni na kuboresha huduma za kibenki kuwawezesha wanafamilia kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki Tanzania ambapo katika kulizingatia hili, mwishoni mwa wiki NMB si imezindua akaunti ya Chap Chap ambayo imelenga kuwafikia wanafamilia wote na kuwafungulia akaunti zao yani unafungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha ndani ya dakika  kumi.
.
Sehemu ya maofisa na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.

      Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na kuona salio la akaunti yako popote ulipo, kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa, kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta, kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu, kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye ATM
.
Ofisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru waziri wa fedha Dk William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap.

Read more »

Yaliyojiri katika Magazeti June 18 2013 za Udaku, Michezo na Hardnews.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Read more »

Sentensi 5 kuhusu Mabomu mengine yaliyolipuliwa na Polisi Soweto Arusha leo June 18 2013

.
Arusha.
Maripota wetu kutoka Arusha wanaripoti kwamba mabomu ya machozi yakipigwa na Polisi yameanza kusikika toka saa kumi jioni kwenye eneo la Soweto.

Mmoja wa maripota hawa amesema wakati alipokua karibu na mkusanyiko huo kuna Askari Polisi mmoja ambae alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa kwa mabomu na kufariki June 15 2013 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.

Baada ya hapo hawa Wafuasi hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka kama kutoelewana huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa huku pia Viongozi wa Chadema wakihutubia…. ndio mabomu yakaanza kusikika.

Ripota wa pili anasema “Baada ya Tundu Lissu wa Chadema kuhutubia na kusema chanzo cha vifo vya June 15 2013 ni Polisi, yani vifo hivyo viliratibiwa na RPC Arusha… mabomu ya machozi ndio yakaanza kulipuliwa”

Mpaka saa kumi na moja na dakika 40 hii post inaingia hapa, wafuasi wa Chadema bado wako maeneo ya Soweto Arusha, wamegoma kuondoka na kusema wanataka kujua kwanza usalama wa Viongozi wao…. lakini pia mabomu yanaendelea kusikika kwenye sehemu nyingine kama Sanawari, Arusha mjini, Mianzini na maeneo mengine.

Read more »