Pages

Wednesday, October 23, 2013

Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu ya Manchester United.


Meneja wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu hiyo kwasababu nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza alidhani yeye ni mkubwa kuliko meneja.
Katika kitabu chake kipya kinachoelezea maisha yake ya ukocha, Ferguson amesema aligombana na Beckham baada ya kumkosoa kwa kiwango chake alichokionyesha katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Arsenal ambao walipoteza.
Katika kitabu hicho Ferguson ameandika kuwa dakika ambayo mchezaji wa United atakapodhani yeye ni mkubwa kuliko meneja ni lazima aondoke na Beckham alidhani yeye ni mkubwa kuliko Ferguson ndio maana akamuuza.
Ferguson pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu mtindo wa maisha ya watu mashuhuri kufuatia nyota huyo kumuoa Victoria Adams aliyekuwa nyota wa kundi la muziki la Spice Girls nchini humo.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Beckham ndiye mchezaji pekee kati ya aliyowafundisha kuchagua maisha ya umaarufu na kitendo hicho hakikumfurahisha ndio maana akamuacha aondoke.
Lakini Ferguson alimpongeza nyota huyo kwa mchango wake uliochangia mafanikio mengi ya United na kumtaja kama kioo cha watoto wote duniani.
Katika kipindi chote cha miaka 26 aliyofundisha United, Ferguson alishinda mataji 38 na kufanikiwa kuwafundisha nyota kadhaa wakiwemo Beckham, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo, Peter Schmeichel, Bryan Robson, Roy Kean, Jaap Stam na Ruud Van Nistelrooy.

Read more »

Wednesday, October 9, 2013

TFF imeendelea kutoa ufafanuzi wa nini na nani yupo katika familia ya soka.

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga
 ****
Wakati kamati ya rufaa ya maadili ikitarajia kukutana leo kwa ajili ya kusikiliza rufaa zilizowasilishwa mbele yake pamoja na kutoa ufafanuzi wa maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya maadili majuma mawili yaliyopita dhidi ya wadau wa soka waliotakiwa kuendelea na adhabu ya kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi mara baada ya kusikilizwa kwa mashauri yao, shirikisho la soka nchini TFF imeendelea kutoa ufafanuzi wa nini na nani yupo katika familia ya soka.


Mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji Alex Mgongolwa amesema tafsiri wa nini na nani yupo katika familia ya soka imekua ikitolewa tafsiri tofauti ambapo hali hiyo inaleta mkanganyiko na kusababisha baadhi ya wadau walioenguliwa katika mchakato wa uchaguzi kujiona hawana haki ya kuwa katika familia hiyo.

Bofya hapa chini kumsikiliza:- MGONGOLWA


Hata hiyo kwa kuonyesha ni vipi suala hilo linavyowachanganya wadau wa soka nchini, bado raisi wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga alipokutana na waandishi wa habari siku mbili zilizopita alizungumza kwa lengo la kufafanua nini chanzo cha kuundwa kwa kamati za maadili kama ilivyoagizwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

 Bofya hapa chini kumsikiliza:- RAIS WA TFF TENGA


Read more »

Monday, October 7, 2013

BABA LEVO ATANGAZA KUBADILISHA JINA NA ADAI BIFU ZA MUZIKI WA BONGO HUPOTEZA WAKATI NA HAZINA MANUFAA.

Hitmaker wa Vuvuzela Baba Levo, amesema Bifu za wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya Tanzania hazina manufaa yoyote zaidi ya kupoteza muda na kibongo bongo bifu lililopo si kwa wasanii wa muziki wa Hip Hop bali ni kwa wasanii wote.

"Bifu hali kwenye Hip Hop tu lipo sehemu yoyote kwa sababu bifu inakuja kutokana na mazingira tunayoishi, kwa mfano Diamond na H Baba wana bifu lakini hawafanyi Hip Hop" BABA LEVO Aliikiambia kipengele cha Chumba Cha Sindano katika Kipindi cha Kali za Bomba kutoka kituo cha redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya. 

Kwa maelezo zaidi sikiliza hapa chini...........

Akizungumzia sababu za kuachana na Muziki wa miondoko ya HIP HOP Baba Levo amesema "Sababu zilizonifanya niachane na HIP HOP au sio bwana, baada na kuona mazingira ya Hip Hop kwangu yanakuwa magumu kupata hela kwa sababu tunafanya music ili tupate pesa, kwa sababu watu wanafanya HIP HOP wanapata pesa lakini kwangu ilikuwa vigumu"

Kwa maelezo zaidi sikiliza hapa chini...........


Aidha Baba Levo amesema kwa sasa amebadilisha jina na kujiita BABA LA BABA LEVO na kuelezea sababu za kubadilisha jina lake ni kutokana na mwanae kumbatiza jina la LEVOCATUS jina ambalo pia ni la baba yake mzazi na uzinduzi wa jina hilo utaenda sambamba na utambulisho wa Ngoma mpya iitwayo Baba la Baba na video mpya ya Boss Mapombe.

Kwa maelezo zaidi sikiliza hapa chini...........

Read more »