Pages

Wednesday, October 23, 2013

Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu ya Manchester United.


Meneja wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alitakiwa kuondoka katika klabu hiyo kwasababu nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza alidhani yeye ni mkubwa kuliko meneja.
Katika kitabu chake kipya kinachoelezea maisha yake ya ukocha, Ferguson amesema aligombana na Beckham baada ya kumkosoa kwa kiwango chake alichokionyesha katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Arsenal ambao walipoteza.
Katika kitabu hicho Ferguson ameandika kuwa dakika ambayo mchezaji wa United atakapodhani yeye ni mkubwa kuliko meneja ni lazima aondoke na Beckham alidhani yeye ni mkubwa kuliko Ferguson ndio maana akamuuza.
Ferguson pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu mtindo wa maisha ya watu mashuhuri kufuatia nyota huyo kumuoa Victoria Adams aliyekuwa nyota wa kundi la muziki la Spice Girls nchini humo.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Beckham ndiye mchezaji pekee kati ya aliyowafundisha kuchagua maisha ya umaarufu na kitendo hicho hakikumfurahisha ndio maana akamuacha aondoke.
Lakini Ferguson alimpongeza nyota huyo kwa mchango wake uliochangia mafanikio mengi ya United na kumtaja kama kioo cha watoto wote duniani.
Katika kipindi chote cha miaka 26 aliyofundisha United, Ferguson alishinda mataji 38 na kufanikiwa kuwafundisha nyota kadhaa wakiwemo Beckham, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo, Peter Schmeichel, Bryan Robson, Roy Kean, Jaap Stam na Ruud Van Nistelrooy.

Read more »

Wednesday, October 9, 2013

TFF imeendelea kutoa ufafanuzi wa nini na nani yupo katika familia ya soka.

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga
 ****
Wakati kamati ya rufaa ya maadili ikitarajia kukutana leo kwa ajili ya kusikiliza rufaa zilizowasilishwa mbele yake pamoja na kutoa ufafanuzi wa maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya maadili majuma mawili yaliyopita dhidi ya wadau wa soka waliotakiwa kuendelea na adhabu ya kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi mara baada ya kusikilizwa kwa mashauri yao, shirikisho la soka nchini TFF imeendelea kutoa ufafanuzi wa nini na nani yupo katika familia ya soka.


Mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji Alex Mgongolwa amesema tafsiri wa nini na nani yupo katika familia ya soka imekua ikitolewa tafsiri tofauti ambapo hali hiyo inaleta mkanganyiko na kusababisha baadhi ya wadau walioenguliwa katika mchakato wa uchaguzi kujiona hawana haki ya kuwa katika familia hiyo.

Bofya hapa chini kumsikiliza:- MGONGOLWA


Hata hiyo kwa kuonyesha ni vipi suala hilo linavyowachanganya wadau wa soka nchini, bado raisi wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga alipokutana na waandishi wa habari siku mbili zilizopita alizungumza kwa lengo la kufafanua nini chanzo cha kuundwa kwa kamati za maadili kama ilivyoagizwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

 Bofya hapa chini kumsikiliza:- RAIS WA TFF TENGA


Read more »

Monday, October 7, 2013

BABA LEVO ATANGAZA KUBADILISHA JINA NA ADAI BIFU ZA MUZIKI WA BONGO HUPOTEZA WAKATI NA HAZINA MANUFAA.

Hitmaker wa Vuvuzela Baba Levo, amesema Bifu za wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya Tanzania hazina manufaa yoyote zaidi ya kupoteza muda na kibongo bongo bifu lililopo si kwa wasanii wa muziki wa Hip Hop bali ni kwa wasanii wote.

"Bifu hali kwenye Hip Hop tu lipo sehemu yoyote kwa sababu bifu inakuja kutokana na mazingira tunayoishi, kwa mfano Diamond na H Baba wana bifu lakini hawafanyi Hip Hop" BABA LEVO Aliikiambia kipengele cha Chumba Cha Sindano katika Kipindi cha Kali za Bomba kutoka kituo cha redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya. 

Kwa maelezo zaidi sikiliza hapa chini...........

Akizungumzia sababu za kuachana na Muziki wa miondoko ya HIP HOP Baba Levo amesema "Sababu zilizonifanya niachane na HIP HOP au sio bwana, baada na kuona mazingira ya Hip Hop kwangu yanakuwa magumu kupata hela kwa sababu tunafanya music ili tupate pesa, kwa sababu watu wanafanya HIP HOP wanapata pesa lakini kwangu ilikuwa vigumu"

Kwa maelezo zaidi sikiliza hapa chini...........


Aidha Baba Levo amesema kwa sasa amebadilisha jina na kujiita BABA LA BABA LEVO na kuelezea sababu za kubadilisha jina lake ni kutokana na mwanae kumbatiza jina la LEVOCATUS jina ambalo pia ni la baba yake mzazi na uzinduzi wa jina hilo utaenda sambamba na utambulisho wa Ngoma mpya iitwayo Baba la Baba na video mpya ya Boss Mapombe.

Kwa maelezo zaidi sikiliza hapa chini...........

Read more »

Tuesday, September 24, 2013

SOGGY DOGGY AITOLEA UVIVU COSOTA & BASATA SIKILIZA HAPA CHUMBA CHA SINDANO YA KALI ZA BOMBA SEPT 24

 

 STORY KWANZA - SOGGY DOGGY.
Rapper Soggy Doggy a.k.a Chief Rumanyika, licha ya kushirikiana na wasanii wenzake D Knob, Sugu na Bwana Misosi kupigania suala la wasanii kupata hati miliki ya kazi zao, Serikali imekuwa ikisuasua kutafuta ufumbuzi wizi wa kazi za wasanii na kwamba itachukua mud asana wasanii kuja kunufaika na kazi zao.


 STORY PILI - SHADAMO.

Upcoming Artist kutoka Green City namzungumzia Shadamo, ambaye pia anafanya vizuri kupitia Track ya MILELE MIMI NA WEWE amewatwatukia wasanii wenzake Undergrounds kujiamini na kujipenda katika kazi zao, licha ya kuwa katika kufikia mafanikio kuna misukosuko ya vikwazo na kutatishana tama, lakini wakitia nia gemu la muziki wa kizazi kipya lina wigo mpana wa mafanikio.

 STORY KAMILI:- KAMA ULIKOSA KUMSIKILIZA MAHOJIANO NA SOGGY DOGGY  NA SHADAMO KATIKA CHUMBA CHA SINDANO ya KALI ZA BOMBA - BOMBA FM 104.0MHz WASIKILIZE HAPA.

Read more »

Monday, September 23, 2013

Ni Di Matteo, McLeish, McClaren takayechukua nafasi ya Paolo Di Canio katika Klabu ya Sunderland.


Majina ya mameneja Roberto Di Matteo , Tony Pulis , Gus Poyet , Alex McLeish pamoja na  Steve McClaren yamekua yakitajwa katika mchakato wa kumsaka mrithi wa meneja kutoka nchini Italia Paolo Di Canio ambae amefungashiwa virago huko Stadium of Light yalipo makao makuu ya klabu ya Sunderland.

Vyombo vya habari nchini Uingereza tangu mapema hii leo vimekua vikiyataja majina ya mameneja hao ambao wanaijua vyema ligi ya nchini humo kwa kusema huenda mmoja wao akapewa ajira na uongozi wa klabu ya Sunderland.

Taarifa hizo zimedai kwamba mameneja wote hao wamekua katika harakati za kutafuta kazi kwa muda wa miezi kadhaa sasa na wapo tayari kuichukua nafasi ya Paolo Di Canio ambae ameionja shubiri ya kutimulia kazi baada ya kushindwa kuanza vyema msimu wa ligi nchini Uingereza.

Hata hivyo katika mlolongo wa mameneja hao Roberto Di Matteo, ambae aliiwezesha klabu ya Chelsea kuandika historia ya kuwa wafalme wa soka mwaka 2012 barani Ulaya, anaonekana kuwa chaguo la kwanza la viongozi wa klabu ya Sunderland ambao bado wanaendelea kujadiliana namna ya kuiziba nafasi ya meneja klabuni hapo.

Paolo Di Canio ambae alipewa ajira huko Stadium of Light mnamo March 31 mwaka huu alifanikiwa kuinusuru klabu ya Sunderland kushuka daraja msimu uliopita baada ya kuikuta ikiwa katika hali mbaya ambayo ilisababishwa na utendaji mbovu wa meneja aliemtangulia Steve Bruce.

Tangu alipoingia klabuni Paolo Di Canio mwenye umri wa miaka 45, alifanikiwa kushinda michezo mitatu pekee kati ya michezo 13 ambayo imeshuhudiwa ikichezwa akiwa kama mkuu wa benchi la ufundi.

Akizungumza mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya West Bromwich Albion ambao ulikua mchezo wa mwisho kwake kama meneja wa klabu ya Sunderland Paolo Di Canio alikiri kikosi chake bado kilikua na matatizo ya kuelewana baina ya mchezaji na mchezaji hivyo ilikua ni vigumu kwake kuanza vyema msimu huu huku wakiwa tayari wameshacheza michezo mitano.

Pia Paolo Di Canio akajitabiria mabaya wakati alipokua akizungumza na vyombo vya habari kwa kusema yeye alistahili kuwajibishwa kwa kosa hilo.


Katika mchezo huo kikosi cha Sunderland kilikubali kisago cha mabao matatu kwa sifuri, na kabla ya hapo walikubali kufungwa na Arsenal mabao matatu kwa moja huku Cryastal palace wakitanguli

Read more »

KAMA ULIKOSA KUMSIKILIZA MAHOJIANO NA JOSLIN, CHRIS WAMARYA, KABAGO, VUMBE NA PNC KATIKA CHUMBA CHA SINDANO - BOMBA FM WASIKILIZE HAPA.

STORY KWANZA - JOSLINHitmaker wa Itika Joslin amesema yeye hajifananishi na Msanii yeyote hapa Bongo, kwa sababu yeye ana ladha tofauti katika ngoma zake ambayo hukatisha kiu ya mashabiki wa muziki ambao wanahitaji kuona uhalisia wa msanii juu ya kile anachokiimba....
 
STORY YA PILI- CHRIS WA MARYA.Hitmaker wa Kilometer 6, Sinyorita na nyinginezo track kibao CHRIS WAMARYA kutoka Mji kasoro bahari, amedai kuwa ataendelea kuimba muziki wenye ladha ya bongo ili hata wasanii wa Kimataifa wapate kuuiga.... 
 STORY YA TATU- CHRIS WA MARYA.Rapper KABAGO wa BMW amesema anamshukuru Mola kwa kumpa uhai mpaka sasa na madaktari walioweza kumtibu haraka  na kumsababishia kuendelea vema, kufuatia ajali iliyotokea Jumapili eneo la Msituni wakati yeye pamoja na wasanii wenzake wakitokea Geita katika show kuelekea Airpot Mwanza.
 
NB:-Pia VUMBE na PNC wameweza kuzungumzia ajali hiyo.

STORY KAMILI WASIKILIZE HAPA WAKIZUNGUMZA:- KAMA ULIKOSA KUMSIKILIZA MAHOJIANO NA JOSLIN, CHRIS WAMARYA, KABAGO, VUMBE NA PNC KATIKA CHUMBA CHA SINDANO - BOMBA FM WASIKILIZE HAPA.

Read more »

MAHOJIANO KWA LUGHA YA KISWAHILI KATI YA MWANDISHI WA HABARI NA MSEMAJI WA AL-SHABAAB JUU YA MAUAJI YA ZAIDI YA WATU 59 JIJINI NAIROBI.


Mwandishi Jamal Osman amefanya mahojiano exclusive na msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kuishambulia mall ya Westgate. 

Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4

Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda. 

Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.

JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?

Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya. 

Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu.
 Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.

JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo.
 Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji. 

Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.

JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?

Msemaji:
 Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.

JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?

Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.

JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?

Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.

JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?

Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.

JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?

Msemaji:
 Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.

JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?

Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.

JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?

Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia.

 Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya

Read more »

Sunday, September 22, 2013

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE MISS TANZANIA 2013

IMEWEKWA SEPTEMBA 22, 2013 SAA 3:40 ASUBUHI
Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kushoto ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania.Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.
 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 
 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.
Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakipita jukwaani na mavazi ya aina mbali mbali wakati wa Onyesho la Taifa Redd's Miss Tanzania 2013 linalofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam usiku huu. 
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013,linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI

Read more »

PICHA ZA KUSIKITISHA KATIKA SHAMBULIO LA KENYA HAPO JANA..!! TAHADHARI BAADHI YA PICHA ZINATISHA.!

September 21, ni tarehe ambayo Kenya haitoisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi na kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine. Mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa akiomba msaada Mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa akiomba msaada Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari 
 Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari article-2427892-182485E800000578-152_964x631 130921145130-25-kenya-mall-restricted-horizontal-gallery 130921103725-07-kenya-mall-horizontal-gallery Mashuhuda wanasema watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na nguo nyeusi na vichwa vyao vikifunikwa na vilemba waliingia kwenye mall hiyo ya Westgate jana mchana. Mpaka sasa, idadi ya watu walioshikiliwa mateka ndani ya mall hiyo haijajulikana. Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatili  
Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatili Mfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo Mfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo Mtoto akikimbia kuokoa maisha yake  
Mtoto akikimbia kuokoa maisha yake
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Zaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa na zaidi ya 162 wakijeruhiwa. Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo hao  
Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo hao Mwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askari Mwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askari Mwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shopping Mwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shopping Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwa Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwa Maafisa wamesema watu hao wamebananishwa na kwamba watu wameshikiliwa mateka kwenye maeneo mbalimbali. Al-Shabab imeliambia shirika la habari la Uingereza BBC kuwa limefanya shambulio hilo kujibu opereshini za kijeshi za Kenya zinazoendelea nchini Somalia. <img src="http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/09/Mwanaume-aliyejeruhiwa-akilia-kwa-uchungu-kutokana-na-maumivu-makali-baada-ya-kupigwa-risasi-ya-mguu.jpg" alt="Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu" width="600" height="400" class="aligncenter size-full wp-image-57459" Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu Ofisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silaha  
Ofisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silaha Polisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mall Polisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mall Polisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao 
 Polisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao Mashuhuda wengine wamedai kuwa wanamgambo hao waliwaambia waislamu waondoke na wabaki waumini wa dini zingine. “Walisema na kusema: ‘Kama wewe ni muislamu, simama. Tumekuja kuwaokoa,” Elijah Lamau aliiambia BBC. Alisema waislamu waliondoka wakiwa wamenyoosha mikono juu na kisha watu hao wakawapiga risasi watu wawili. Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-Shabab 
 Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-Shabab Polisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-Shabab 
 Polisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-Shabab Polisi wakipambana na Al-shabab 
Polisi wakipambana na Al-Shabab Rais wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi hao  
Raia wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi hao Wanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-shabab Wanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-Shabab Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameimbia BBC kuwa wengine wanne wamekamatwa. Wananchi wakikimbia kuokoa maisha yao Wananchi wakikimbia kuokoa maisha yao Wanawake na watoto wao wakihaha kuokoa maisha yao ndani ya mall hiyo Wanawake na watoto wao wakihaha kuokoa maisha yao ndani ya mall hiyo Wanawake waliojeruhiwa wakisaidiwa Wanawake waliojeruhiwa wakisaidiwa Watu mbalimbali wakijaribu kuokoa maisha yao wakati watu hao wenye silaha wakiwa ndani ya mall  
Watu mbalimbali wakijaribu kuokoa maisha yao wakati watu hao wenye silaha wakiwa ndani ya mall Watu wakimsaidia kumdaka msichana aliyekuwa amejificha ndanii ya mall hiyo  
Watu wakimsaidia kumdaka msichana aliyekuwa amejificha ndanii ya mall hiyo Watu wakisaidiwa kutoka nje ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa  
Watu wakisaidiwa kutoka nje ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa Watu waliokuwa ndani ya Westgate wakisaidiwa kutoka nje na askari  
Watu waliokuwa ndani ya Westgate wakisaidiwa kutoka nje na askari Watu waliokuwa wakifanya shopping wakisaidiwa kutoka nje ya mall na askari  
Watu waliokuwa wakifanya shopping wakisaidiwa kutoka nje ya mall na askari
Source: Bongo5

Read more »